Mo Faya ya Alikiba Kudhamini Matangazo ya Kombe la Dunia.
Msanii wa bongo fleva Alikiba siku ya jana aliungana na mashabiki na watu wengine katika uzinduzi wa matangazo ya kombe la Dunia mwaka huu kupitai DSTV ambapo akiwa kama bosi wa Mofaya Alikiba na kampuni yake pia watahusika katika kudhamini matangazo ya mpira kupitia channel mbalimbali za kombe la Dunia.
Akiongea na waandishi wa habari wa clouds E , Alikba ansema kuwa pamoja na kwamba ndio anaanza lakini haoni kukatishwa tamaa na uamuzi huokwa sababu kwake ni swala la kujivunia kuwa moja ya wadhamini katika matangazo hayo.
Nikiwa kama msanii najivunia sana na mo faya kuwa mdhamini wa matangazo haya ya kombe la dunia katika channel za dstv, tunachotakiwa sio kuvunjika moyo lakini kujaribu kufanya kitu kwa ajili ya kuendeleza na kuwafikia mashabiki wetu.