Hatimaye Shilole apata mwanaume wa kumuoa

Kuna fununu kwamba Shilole amepata mchumba kulingana na magazeti wanavyosema mitandaoni. Mrembo huyu ambaye ameweza kuwa na wanaume kadhaa bongo hatimaye amepata mtu ambaye anamtuliza kiroho na kiakili.

Kulingana na Global Publishers Shilole amempata mwanaume mchumba ni dereva wa bodaboda Kinondoni. Waliendelea kusema kuwa chanzo cha habiri hizi kilikiri kuwa Shilole na mchumba wake wanatarajia kufunga ndoa ya siri kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanza.

“Shilole anatarajia kufunga ndoa na dereva bodaboda hivi karibuni kabla Waislamu kuingia kwenye Mfungo wa Ramadhan na itakuwa ya siri, nyie fuatilieni mtaujua tu ukweli,” kilisema chanzo.

Hata hivyo Shilole ambaye aliweza kuongea na wanahabari alisema kuwa ni kweli kuwa amepata mchumba lakini akikataa kumuweka wazi kwa sasa. Aliendelea kwa kusema kuwa Mchumba wake siyo siyo dereva wa bodaboda kama watu wanavyosema.

“Ni kweli nina mchumba, ila siyo dereva bodaboda, ni fundi magari, tuko kwenye utaratibu wa ndoa na nitawajulisha maana ndoa yangu haitakuwa ya siri, itakuwa ya wazi na itafungwa kwenye ndege,” alisema Shilole.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.