Shetta hatimaye awajibu mashabiki wake

Msanii wa bongo Shetta aliachia ngoma yake mpya ‘Wale Wale’ hivi karibuni na kulingana na YouTube inaonekana kuwa Shetta aliangusha wimbo ambao umewaacha mashabiki huku kama wamefurahi.

Hata hivyo, Shetta ameonekana kuwajibu mashabiki wanaodai asikae kipindi kirefu bila kutoa ngoma.

Shetta

 

Hii ni baada ya kukawia zaidi ya miezi 10 bila  kutoa wimbo. Akizungumza na E-Newz ya EATV Shetta alisema;

“Mimi naamini katika kitu ambacho nakifanya, nimeshauriwa nifanye back to back lakini hata hiyo itaongezeka ngoma moja au mbili, sidhani kama natakiwa nifanye vitu ambavyo watu wanasema au wanafikiri ni sawa, mimi natakiwa niamini katika kitu ambacho nafanya,”

Aliendelea kwa kusema;

“Lakini kutokana mashabiki wanataka pia nafuata kile wanachopenda nitajaibu kubadilika ila katika moyo wangu siamini katika kutoka nyimbo nyingi. Bajeti pia huwa inabana kutokana kitu ninachotaka kukifanya pia ni kikubwa,”

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.