Diamond Aongelea Jinsi Alivyombembeleza Zari Asimuache

Mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa msanii aliyeshika vichwa vya habari kwa takribani miezi miwili mfululizo kuanzia skendo yake ya kuzaa na Hamisa mpaka kuachana na Zari na mengine Mengi yaliyozuka hivi kati.

Diamond aliongelea uhusiano wake na Zari alipokuwa jukwaani siku ya Jumamosi alipopiga shoo kwenye uwanja wa Amani, Zanzibar ambapo Diamond alisema:

Unajua hapa katikati palitokea mambo mambo mengi, shetani akaingia kati mara maneno ooh hivi na vile ebwana mambo yakawa mengi kweli unajua, nikaona enhee mtoto wa kiganda kacharuka, nikiangalia kushoto na kulia nikawa naona kabisa kama jiko nakaribia kulikosa moja kwa moja nikapanda ndege nikaenda mpaka Sauzi, kufika sauzi kabla hata sijaongea moja kwa moja mpaka chumbani kule tulifanya vitu vingi sana nikajua mambo yatakuwa yameisha, hee mambo yakaendelea nafika tu Tanzania yakazuka mengine, akanitupia dongo kwenye Instagram nikapiga simu takribani saa zima nabembeleza baby anisamehe nikamwambia baby sikia hivi vitu vinatokea mi nimeteleza nikamuimbisha mtoto mgumu hataki kusikia mpaka ilivyonijia nyimbo kwenye kichwa nikamwimbia mtoto ndo ameelewa”.

Pamoja na yote yaliyotokea baina yao Diamond amekiri kuwa Zari kamsamehe na wamerudiana na wanataka kuendelea kulea watoto wao na kutengeneza pesa.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.