Diamond Atoa Fursa ya Vipaji vya Utangazaji Bongo

Wakati bado wanasubiri kuwasha mitando ya radio na televishei zao kwa ajili ya kazi zao na kazi za wasanii wengine ili kukuza soko la muziki Tanzania, meneja wa lebo ya wcb Diamond Platinumz anaonekana bado ana nia ya kutoa fursa na ajira kwa watu wengine ambao sio wasanii katika vituo hivyo vya habari.

Diamond na lebo yake ambao wamepanga kufanya mapinduzi ya muziki kwa kutaka kufungua radio na televisheni kwa ajili ya kazi za wasanii, ameamua kutoa fursa ya utangazaji kwa vijana wa Tanzania katika stations hizo.

Katika ukurasa wake wa instagram, Diamond Platinumz aliandika “please tell me from you perspectives,which cuty has the best radio and tv presenter,….eti nina swali ni mkoa gani ambao una vipaji vya utangazaji.-Aliandika Diamond.

Diamond anaweza kuwa ni moja ya wasaniiwachache afrika ambao wanataka kukuza muziki tanzania lakini ni mtu mwenye moyo wa kusaidia vijana wenguen wa nyanja tofauti tofauti.ukiachana na kutaka kufungua radio na televisheni, Diamond alishafanikiwa katika kufungua lebo hiyo ya wcb na kutafuta wasanii chipukizi kwa ajili ya kuwasaidia kuinua viapji vyao.

Wasanii ambao mpaka sasa wamekuwa chachu ya mafanikio ya muziki kwa wasanii wengien kutokana na kazi nyingi na nzuri wanazofanya za kukuza na kuutangaza muziki nje ya Tanzania.

Baadhi ya wasanii wanaopatikana katika lebo ya diamond ni pamoja na Rayvanny, Harmonize na Lavalava.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.