Siri Imevuja, Mwanakher Aolewa Mke wa Pili.
Wikiend iliyopita kulisambaa kwa picha za mwanadada Mwanakheri anaefanya vizuri katika tasnia ya movies bongo kuwa amefunga ndoa huku ikisemekana kuwa sio watu wote waliokuwa wanajua kuwa mwanadada huyo ameolewa mpaka picha zilipoanza kusambaa.Sasa siri imekuja kujulikana kuwa mwanadada huyo aliamua kufanya kwa siri kwa sababu mwanaume aliyemuoa ni mue wa mtu na mwanaume huyo hakutaka mke wake kujua swala hilo la ndoa.
Chanzo cha habari hii ambae ni mtu wa karibu wa Mwanakheri alipokuwa akiongea na Global Publishers alifunguka na kusema kuwa mwanaume aliemuoa Mwanakheri ni mume wa mtu na ba awa familia yake na watoto na ni moja ya wafanyabiashara wakubwa bongo.
kama hamna ubuyu ni kwamba mwanaume aliyemuoa anandoa na watoto na ndio maana aliamua kufanya kimyakimya bila ya watu wengi kujua, kitu kingine wasichokijua ni kwamba mwanaume aliyemuoa anamzidi umri kwa kiasi kikubwa sana.
Hata hivyo mwanakheri alitafutwa na global kuulizwa juu ya swala hilo ndipo aliposema kuwa aliamua kufunga ndoa harakaharaka kwa sababu mume wake alikuwa na safari ya ghafla, na kuhusu swala la mwanaume kuwa na familia Mwanakheri anasema kuwa anachojua yeye ni kuwa mume wake ana watoto tu basi na swala la kuzidiwa umri yeye haangalii ilo anachoangalia ni ndoa yenye staa tu basihayo mengine hawezi kuyasemea.