H.Baba- Hakuna Msanii Wa Kushindana na Mziki Wangu

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva H.baba amefunguka na kudai mpaka hivi sasa hajaona bado msanii ambaye anaweza kushindana naye.

H.baba ameweka wazi kuwa ukimya wake Kwenye gemu unatokana na yeye kukosa msanii ambayr anaweza kushindana naye kwani mziki wake ni wa kipekee.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, H.baba  amesema ameona akae pembeni kwa muda kuwa muziki wa BongoFleva unaenda kupotea kabisa kwenye ramani nchini Tanzania.

Mimi binafsi naona muziki unaelekea ukingoni, wasanii wameacha kufanya muziki wanafanya kiki kila kukicha.

Sisi tulipendwa kutokana na muziki wetu na sio makiki yasio na mpango ndio maana baada ya kuona sina mshindani tena nikaamua nikae pembeni siku akitokea mshindani wangu mtaona fujo zangu”.

H.Baba amedai kwa sasa anashindwa kuweka wazi ni lini ataachia wimbo wake mpya kwa madai anaogopa kulogwa kwani wasanii wa siku hizi wanatumia ndumba kuwashusha kimuziki wasanii wenzao.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.