Emmanuel Mbasha Akumbwa na Skendo za Kuazima Magari

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha amefungukia tuhuma alizotupiwa hivi karibuni na kudaiwa kuwa anapenda kuazima magari.

Habari za chini chini zilisambaa kuwa Mbasha ni mmoja kati ya mastaa  ambao wanaazima magari ya watu na kisha kuyaanika Kwenye mitandao ya kijamii kama yao.

Mbasha amekana tetesi hizo na kudai kuwa taarifa hazina ukweli wowote kwani magari yote ambayo anayaweka Kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mbasha amesema kuwa yeye sio muuza sura na magari yote aliyokuwa nayo ana uwezo wa kuyamiliki kutokana na kwamba  kazi yake inamuingizia kipato cha kutosha.

Hamna, mimi huwa siazimi magari, yote niliyona ni ya kwangu, ninatumia gari zangu na watu wa karibu yangu wanafahamu mimi ni mfanyabiashara, ninaimba Gospel na nina kipato cha kufanya mambo yangu yote ya unayoyaona“.

Mbasha alijizolea umaarufu Kwenye muziki wa Injili Tanzania baada ya kufunga ndoa na mwanamama aliyekuwa anafanya vyema Kwenye sekta hiyo Florah Mbasha ambaye kwa sasa wameachana.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.