Kala Jeremiah Atoa Sababu za Kufanya Kazi na Walter Chilambo.
Msanii Kala jeremiah amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa iliyomfanya akamchagua msanii mwenzake Walter chilambo katika wmbo wake uanaokuja ambao unaitwa Natabiri ambao utatoka hivi karibuni na kusema kuwa amekuwa akmjua walter kwa muda mrefu hivyo anaona hajakosea kufanya hivyo.
Kala anasema kuwa kwa jinsi wimbo ulivyo, unahitaji mtu ambae atakuwa na nidhamu na muonekano wa kidini na kwa msanii walter anaweza kabisa kufit katika nafasi hiyo.
sababu ya mimi kumshirikisha waletr ni kwa sababu kwanza ana uwezo mkubwa tu wa kuimba, namjua vizuri na nimekuwa nikimfatilia vizuri,lakini pia nilitaka kupata mtu atakae endana na maudhui ya wimbo , wimbo una maudhui ya kidini na kiimani kwaio ukiusikiliza mwenyewe unajua kwanini walter.
lakini pia tuna historia ya mimi na walter wote tumetokea katika bongo star search , kwaio utakuwa ni wimbo wa kwanza wa washindi wa bongo star search kwa mara ya kwanza na ukisikiliza chorus aliyopiga huyo jamaa utaona jinsi mtoto anavyojua kuimba na kumjua walter.
Kwa miaka tofauti wasanii hawa wote wawili waliwahi kushiriki katika mashindano ya BSS yanayofanyika nchini kutafuta vipaji vya uimbaji, hii itakuwa ni moja ya historia ya mafanikio kwa wasanii na washindi wa shindano hili.