Mimi na FA Nahisi Tunaenda Sana:-Alikiba
Miaka kadhaa iliyopita waliwahi kufanya kolabo ya pamoja iliyokwenda kwa jina la Kiboko Yangu ambayo ilifanya vizuri na kuwafanya kuwa marafiki kwa muda mrefu , hii yote ni kutokana na ufundi waliokuwa nao wote wawili lakini pia kwa sababu wawili hao walikutana na kuelewana kutokana na hekima walizokuwa nazo.
Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa inawezekana kabisa kuwa yeye na Mwana Fa wanaendana sana kwa tabia na baadhi ya vitu katika maisha na inawezekana hii iliwafanya wakafanya kazi na kufanya vizuri siku za nyuma.
Mimi na Mwana FA nahisi kama tabia zetu zinafanana na kuendana , kwa sababu mwana FA yuko ‘real’ sana kwa sababu kama hakuwahi kukukubali basi itakuwa vigumu kukubalika tu,
Siku kadhaa nyuma zilizopita Alikiba aliwahi kusema kuwa katika maisha yake kama hamkubali mtu hamkubali na huwezi kulazimisha hakukubali kwa sababu wakati yeye anahangaika hakuna aliyekuwepo kumsaidia kwa chochote.