Baba Kanumba Aomba Akumbukwe Kwenye Urithi wa Mwanae.
Baba mzazi wa marehemu Steven Kanumba ametuma salamu kwa waziri wa habari, tamaduni na michezo Mh Mwakyembe kwa kumuomba amkumbuke katika mali za Kanumba ambazo zinaanza kushughulikiwa hususani mikataba yake aliywahi kusaini alipokuwa hai.
Siku kadhaa nyuma zilizopita , Mh Mwakyembe alitamka bungeni na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakufanya usainishaji wa mikataba na watu lakini wamekuwa wakishindwa kuendelea na msiah yao kutokana na kwamba wanakuwa wanakosa kujua kle wanachokisaini kitawanufaishaje.
Hivyo basi baba wa marehemu nae ameomba kukumbukwa katika mali hizo endapo zitapatikana kama livyoahidiwa na mh waziri.
Namuomba sana mwakyembe anikumbuke sana katika kusaini fedha za mikataba ya mwanangu endapo zitatoka, kwa maana hata mimi nina haki kwa sababu nilimlea sana tangu akiwa mdogo mpaka mkubwa na ndipo nilipomuuliza anachagua kuka awapi akaniambia anataka kukaa kwa mjomba wake.kwa sasa nimekuwa mlemavu wa miguu hvyo naomba na mimi nikumbukwe sana, nina haki msinisahau.