Irene Uwoya Aapa Kutoifuta Tatoo Ya Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakuja kuiguta tatoo ya marehemu Masogange aliyekuwa rafiki yake kipenzi.

Agnes Masogange aliaga dunia mwezi uliopita baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa pumu enzi za uhai wake yeye na Uwoya walikuwa marafiki wakubwa sana.

Mara baada ya tu ya Agnes kufariki Irene Uwoya alienda kucheza tatoo Kwenye mkono wake kwa ajili ya kumkumbuka shoga yake huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  Ijumaa Wikienda Uwoya amefunguka kuwa aliichora tatoo hiyo kwa kuwa ni jambo lililotoka moyoni mwake na lilitokana na uchungu aliokuwa nao wa kupitiliza kwa rafiki yake huyo hivyo hawezi kuifuta.

Nitaanzaje kuifuta? Ni kitu ambacho nime-kichora mwen-yewe, tena cha kumbukumbu muhi-mu kwenye maisha yangu, jamani itaendelea kudumu kwenye mkono wangu daima“.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.