Uchebe Afafanua Kuhusu Picha ya Irene Katika Akaunti Yake.
Mume wa mwanadada Shiloleh ametoa ufafanuzi juu ya picha ya Irene ambae ni video vixen iliyowahi kupostiwa katika ukurasa wa instagram wa Uchebe na kuandikwa “my bae” na kuwafanya watu kutokwana na mapovu na kuhoji sana juu ya swala hilo.
Akielezea kuhsu tukio hilo, uchebe amesema kuwa akaunti yake ya instagram ilikuwa hacked na watu wasiojulikana na kuanza kufanya vitu hivyo na wala sio yeye na pia yeye hapendi kiki kutokana na kwamba yeye sio msanii na hata kumjua yeye ilikuja kutokana na mke wake.
Katika ukurasa wake wa instagra, uchebe aliandika ” ndugu zangu namashabiki wa mke wangu, mimi sio msanii na mmenijua mimi kupitia mke wangu , mambo ya makiki mimi siyajui na wala siwezi kufanya hivyo.akunti yangu ilichezewa na samahani kwa tafrani , mimi wala siwezi kufanya hivyo.ASANTE SHEMEJI Mxcarter kwa kurudisha akaunti yangu.”