Barakah The Prince Hana Mpango Wa Kuwa Chini Ya Label Yoyote Tanzania

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Baraka The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa hivi sasa hataki kuwa chini ya Label yoyote nchini Tanzania.

Barakah anaweza akawa mmoja kati ya wasanii ambao wameshama hama Label kadhaa hapa nchini kwani ameshafukuzwa na kuacha mara kadhaa na mwishowe ameamua kufungua label yake mwenyewe.

Moja kati ya Label maarufu ambayo Barakah aliwahi kuwepo ni 4000 Rockstar iliyo chini ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba lakini alihama mwaka jana na kudai hakupata maslahi.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari  Barakah anaweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kusainiwa katika label yoyote hapa nchini Tanzania:

Kwa Tanzania hakuna mtu yoyote anayeweza kunisainisha mkataba nikawa chini yake, sijafikiria hilo na wala halitokuja kutokea na hakuna mkakati wa mimi kusainiwa na mtu yoyote”.

Barakah The Prince ameanzisha Label yake mpya akishirikiana na mpenzi wake Naj inayoitwa ‘BaNa Recording Label’ ambayo pia inasimamia kazi za  wasanii kadhaa.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.