Nay wa Mitego ni Mtoto Mdogo Kwangu:-Yusup Mlela
Msanii wa bongo movie Yusup Mlela anaingia tena kwenye headlines baada ya kutamka kuwa hawezi kushindwanishwa na msanii wa bongo movie nay wa mitego hata kidogo kwa sababu Nay ni mtoto mdogo sana kwake.
Nay wa mitego ambae mara nyingi amekuwa akiingia katika migogoro na wasanii wenzake mara nyingi , amekuwa akigombana sana na watu na kuonekana kuwa yeye ni mbambe kila siku kitu ambacho yeye mwenyewe anapinga na kusema kuwa ni kwa sababu amekuwa akisema ukweli kwa wasanii hao.
Hata hivyo yusup mlela anasema kuwa nay wa mitego aache kugombana nae na ajitahidi sana kufanya kazi zake za muziki ili kujiinua zaidi.
Nay wa mitego ni mtoto mdogo tu kwangu,siwezi kushindana nae , ninachomshauri tu aendelee tu kukazana kwenye kazi zake za muziki.