Steve Nyerere Kufunga Ndoa na Wellu Sengo

Mchekeshaji na msanii wa Bongo movie Steve Nyerere ametangaza ndoa na binti Mrembo wa Bongo movie na mzazi mwenzake Wellu Sengo katika siku zijazo.

Global Publishers wanaripoti kuwa Steve Nyerere alitangaza habari hiyo njema Kwenye Ujumbe wa Alfa uliopo Morocco jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya harusi ya msanii mwenzake Jimmy Mafufu.

Katika hali ya utata Steve ametangaza ndoa na Wellu Sengo lakini tayari yupo Kwenye ndoa na mke wake na kudai kilichotokea baina yake na Wellu ni ajali kazini.

Siku ya harusi ya Jimmy Mafufu Steve Nyerere alisimama na kuongea ambapo alifunguka:

Samahani kwanza, naomba kuuliza, “hivi Wellu yumo humu? Mama ndoa yetu na sisi inakaribia anza kujiandaa”.

Baada ya Kauli hiyo iliyoashiria Steve yupo tayari kumuoa Wellu, Mke wa Steve alitoa Kauli yake juu ya suala hilo na kudai:

Steve ataenda popote lakini atarudi tu, kuna wadada wenye maisha magumu wanataka kuwa na maisha bora ndiyo maana wanamsumbua sana mume wangu“.

Miezi michache iliyopita Steve Nyerere alikiri kufanya makosa kuzaa nje ya ndoa na Wellu lakini akasema hana mpango wa kumuoa:

Ni kweli nimezaa na Wellu lakini watu lazima wajue kwamba kuzaa na mtu siyo kuoa, hivyo sidhani kama nitamuoa Wellu“.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.