Wema Sepetu Amvaa Hamisa Kuhusu Tuhuma za Uchawai.
Mwanadada Wema Sepetu amemtupia lawama kubwa Hamisa Mobeto baada ya mwanadada huyo kukumbwa na skendo ya kuwa amekuwa akitaka kuiloga familia ya msanii Diamond ambae ni baba wa mtoto wake wa kiume.
Akiandika waraka mrefu katika ukurasa wake wa instagram, Wema Sepetu anasema kuwa Mange kimambi alipswa kuwa mshauri mzuri kwa hamisa na sio kumfanya mpaka anakwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya mambo yake.
Huku akimcheka kuwa ameshindwa kufanya vitu vyake kwa siri mpaka amebambwa Wema sepetu pia anakataa kujihsisha na kitu chochote ambacho kinahusiana na Hamisa ilhali mashabiki wanamwambia kuwa kama angetaka asiingizwe huko basi alipaswa kutujihusisha tangu zamani.
kwa madai ya Wema ni kwamba mange kimambi amekuwa akimdantanya hamisa na kwamba amekuwa hampi ushauri mzuri kuhusu maisha yake na nini cha kufanya ili kufanikiwa, lakini pia wema anasema kuwa kwa hamisa hata afanye nini pamoja na uchawi wake hatkaa haweze kufika level zake.
…….Usimdanganye huyo mtoto mchawi kuwa anaweza kuwa mimi hata siku moja,,, hawezi na hatokaa haweze tu..medharirika na itabaki kuwa hivyo…aibuuuuuuuuuuuu sana Mungu wangu.. yaaan hata azikiri u*** hawezi