Kuongezeka kwa Mwili Wangu Hakujaathiri Chochote katikaKazi Zangu :-Linah Sanga

Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa swala la kuongezeka kwa mwili wake baada ya yeye kujifungua hakuathiri kazi zake kwa sababu anaweza kufanya kitu chochote jukwaani kuwafurahisha mashabiki wake,

Hii inakuja baada ya moja ya picha yake ya wikiendi hii kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kama amenenepa sana na kuwa anaweza kushindwa kufanya show nzuri kama zamani,

Akiongea na mtandao wa Clouds fm Linah anasema “mazoezi nayafanya ya kawaida tu, naupenda sana mwili wangu.mimi naona kawaida tu na kuongezeka kwa miwli wangu hakujaathiri chochote katika kazi zangu, napiga show jukwaani na najona mwepesi tu.unajua kuna watu ni wembamba lakin wazito lakini mimi unene wangu haujanipa changamoto yoyote.ninapokuwa jukwaani nawaburudisha mashabiki wangu kama kawaida, lakini ujue pia kuwa mimi sio dansa  naimba nitakavyo sio lazima nianze kuruka ruka,’

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.