Mose Iyobo Afunguka Baada Ya Kukamatwa na Polisi

Dansa maarufu kutoka kwenye kikundi cha muziki cha WCB ambaye pia ni mzazi mwenzake na staa wa Bongo movie Aunty Ezekiel, Mose Iyobo amefunguka na kueleza masahibu yaliyowapata baada ya kukamatwa na polisi.

Iyobo na timu nzima ya WCB walikamatwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wakielekea mkoani Mtwara kwenye Tamasha la Wasafi Festival 2018 lililofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Iyobo amesema wakiwa kwenye msafara wa zaidi ya magari 8 ya WCB na wasanii wenzao, alijikuta akidakwa na polisi baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuendesha gari kwa mwendokasi zaidi kuliko uliyoruhusiwa.

Mnenguaji huyo amedai baada ya kukamatwa alikuwa akibishana na askari na kushindwa kuelewana nao, ilisababisha awekwe ndani kwa takribani saa 9 kisha baadaye kuachiwa baada ya kulipa faini.

Ujue tulikuwa tukiwahi kwenye shoo, tukitaka tufike haraka huku mzuka ukiwa mkubwa, kwa hiyo nilikuwa nakanyaga mafuta tu, sikufahamu kama eneo lile sikutakiwa kukimbia kwa spidi kubwa, walinikamata kutokana na kutoelewana nao wakanishikilia. Lakini baadaye waliniachia na shoo tulifanya vizuri“.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.