Sijawahi Kubadilisha Dini Yangu na Kuwa Muislamu-Irene Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu ambao wamekuwa wakimhoji kuhusu kubadilisha dini Baada ya kuachana na Dogo Janja.

Mwaka jana Dogo Janja na Irene Uwoya walishangaza dunia Baada ya kutangaza wamefunga ndoa na kusema Uwoya amebadili dini amekuwa Muislamu na hata jina lake ni Sheila lakini Baada ya kuachana na Dogo Janja amesema hajawahi kubadilisha dini yake ya Kikristo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Uwoya amesema kwa muda mrefu amekuwa akisema kuwa hawezi kubadili dini yake ya Kikristo hivyo watu wafahamu kuwa yeye ni Mkristo na waondoe dhana kwamba alikuwa dini nyingine tofauti.

Nawashangaa sana watu kila kukicha wananiuliza umerudi kwenye dini yako ya awali kama kuna siku hata moja nilishawahi kuwaambia kuwa nimebadilisha dini yangu ya Kikristo yaani siwezi na sijawahi kujaribu”.

Dogo Janja na Uwoya waliachana mwezi uliopita Baada ya tetesi kusambaa kwamba Dogo Janja alichepuka na Msanii Wema Sepetu wakati yupo kwenye ndoa na Uwoya.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.