Afande Sele Alia Na Mpoto,Ni Kuhusu Christian Bella na Uzalendo.

Msanii mkongwe wa muziki tanzania ambae kwa sasa anaonekana kupumzika kufanya kazi hiyo maeibuka juzi na kumvaa msanii mwenzie mkongwe pia , Mrisho Mpoto kuhusu wimbo wa uzalendo ambao uliimbwa siku ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanzania ambapo wasanii wa kizazi kipya  wali-perfom wimbo wa uzalendo wa nchi katika viwanja vya jamhuri   mjiji Dodoma.

Hata hivyo Afande Sele anamlamikia Mpoto kwa madai kuwa alitoa baadhi ya wasanii na kumuweka Christian Bella ambae sio mtanzania na kuacha  wasanii wa kitanzania  na kumwambia kitu hicho sio uzalendo hata kidogo.

Rafiki yangu Mpoto kama kweli wewe ndie uliekuwa kinara katika  katika utayarishaji wa wimbo maalum wa kuhamasisha  uzalendo   kwa taifa na bado ukaweza kushawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii  wazawa na kuweza kumpa nafasi hiyo rafiki yetu Christian Bella kushiriki katika wimbo huo unaowahusu watanzania ilihali unajua fika kuwa rafikiyetu bella   ni kweli kuwa ni rafiki yetu lakini sio  mtanzania bali ni mcongoman.

Kwa mujibu wa Afande Sele anaona kuwa Christian Bella hana haki ya kuimba wimbo huo kutokana na uraia wake na kwamba waliondolewa katika wimbo huo walipaswa kupewa nafasi kubwa kuliko yeye.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamemjia juu mwanamuziki Afande Sele na kumwambia kuwa pamoja na kwamba Bella ni mkongo lakini bado anafanya vizuri katika kukuza muziki wa Tanzania kwaio huo pia ni uzalendo na kama angejijua kuwa hastaili kuimba wimbo wa uzalendo wa taifa lingine angekataa lakini kwa sababu ya uzalendo ndio maana alikubali kuimba.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.