Agnes Masogange apewa onyo na Hakimu Mkuu baada ya kuchelewa kuwasili Mahakamani wakati unaotakiwa

Agnes Masogange ni mmoja wa Video vixen ambao wanajulikana sana Afrika Mashariki. Ameweza kufeature katika video kadhaa nchini Tanzania lakini hivi sasa yuko matatani na Mahakama baada ya kudaiwa kuwa mmoja wa watu maarafu anayetumia madawa ya kulevya.

Mwezi Februari aliweza kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo aliposomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza na kama wengi alikana na mahakama ikabidi kuhairisha kesi yake hadi, March 21, ili kuwapa polisi mda wa kutosha kufanya upelelezi wao.

Video vixen huyu anakabiliwa na mashitaka ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Hata hivyo Jumanne hii mrembo huyu hakuwa mahakamani kuskiza kesi yake baada ya kuchelewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilibidi kutaja kesi hiyo ingawa hakuwa.

Wakili wa Masogange, Nictogen Itege, aliweza kumtetea Masogange huku akisema kuwa yuko njiani. Masogange alipowasili Hakimu Mashauri alimtaka mshitakiwa kutii sheria anazopewa na Mahakama huku kesi yake ikihairishwa hadi Aprili 20, mwaka huu kwa kutajwa.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.