Aina za Kuachana Katika Mahusiano
Katika mahusiano kuna vitu vingi vinaweza kutokea na kusababisha kuachana kwenu, wapo wanaoachana kwa kugombana hata kuchukiana kabisa na wapo wanaoamua tu kuwa sasa mapenzi yanafika mwisho.Hivyo basi kuna aina mbalimbali au Style tofauti za kuachana kwa wapenzi katika mahusiano.
kuachana kwa mlipuko.
kuna kipindi mapenzi yanaweza kutawaliwa na amani sana na mkawa na furaha ya muda mrefu lakini ghafla likatokea tatizo kubwa mabalo linaweza kuwa halina uvumilivu kabisa katika mapnzi yenu hivyo kuwafanya mmoja wenu au wote kuamua kucahana na kila mtu kuanza maisha yake mapya, kwa mfano mmekuwa katika maushiano ya muda refu ghafla mmoja wenu anagundua kuwa kumbe kulikuwa na mahusiano ya muda mrefu huko nje na ukashindwa kutoa sababu ya kueleweka kulingana na ushahidi uliopatikana , hapa mahusiano yanwez kufa kabisa.
mahusiano kuchemka hadi kumwagika.
hapa tunaangalia jinis makwazo ya muda mrefu yanawez akukufanya ukaamua kufanua maamuzi yasiyo sahihi lakini yakawa sahihi kutokana na uvumilivu wa pande moja ya penzi.Ebu fikiria kama mmekuwa kila siku mna mikwazuro modogo midogo isiyoeleweka na hata mwisho kikatokea kitu kidogo sana ambacho kinaweza kuwa kimekukwaza , hapo unaanza kukumbuka na makwazo ya nyuma na kwa sababu makwazo hayo yamekuwa mengi kwa muda mrefu, mapenzi yanakuwa yamesiha tangu siku nyingi hivyo inakuwa rahisi kuachia ngazi.
Off and on style of love
watu wengi sana wamekuwa na styke hii ya mapenzi siku hizi, unakuta kuna muda kunakuwa na mapenzi sana kati yenu alafu baadae mnaachana na kukaa kimya hata miezi kadhaa , alafu baadae mnarudiana tena na kuanza penzi jipya , hii inaweza kuwatokea hata zaidi ya miaka.Tabia hii inaweza kuendelea kwa muda na hata baadae unakua mmoja anpata kitu cha kumwambia kuwa off ya sasa inaweza kuwa ya moja kwa moja na hivyo aanaamua kuachana na mpenzi wake huyo, wakati yule mwingine akiwa anasubiri kurudiana kwao kumbe mwenzake tayari amesha-move on.
Mara moto mara baridi
Kuna watu wanaingia katika mapenzi na kuwa na mahaba mazito sana ya kuwashangaza watu na hata kufanya vitu vikubwa kwa muda mfupi, unakuta mapzni yenu yameanza ghafla sana na kujikuta yanapaa juu sana kiasi kwamba unakuwa na hisia zisizo za kawaida lakini ghafla mapenzi yanakatika na kuisha kabisa.
Mfano, mnaanza mapenzi ghafla na mtu alafu mnakuwa watu wa kuonana kila siku, kuwasiliana kila dakika, kujuliana hali na muda wote mkionana mapenzi yenu ni moto moto, lakini ghafla ukipiga simu haipkelewi, au kule kuonana kunapungua ghafla, kuongea kwa muda mrefu kunapungua ghafla , sasa basi hapo kama hali hiyo itaendelea kwa muda basi mmoja huyo ujiona anateseka na hivyo kukataa tamaa na kuachana na mpenzi wake huyo.
Nafasi iliyosahaulika katika mahusiano.
katika maisha ya mapenzi hakuna kitu kama mazoea, kuna muda hasa kwa watu walioon wanakuwa na tabia ya mazoea kuwa kila kitu kitakuwa sawa na kusahau kuwa unapokuwa jikoni unapika maharage ni lazima kuchochea moto na kuongeza maji pia ili maharage yaive, wengi wanasahau kuchochea kuni, kuongeza maji na kufunikia kabisa ili kuive.mahusiano ya aina hii mwisho wake huwa ni kuachana kwa sababu mahusiano yanakuwa hayana ile radha ambayo ilikuwpo mwanzo na yote haya yanasababishwa na kujisahau kwa waili hao nafasi zao katika mahusiano.