Alichoandika Chid Mapenzi Kuhusu Mke Wake
Mara nyingi amekuwa sio mtu wa kuongea sana kinapotokea kitu chochote hata kama kitu hicho kinamhusu yeye, mara nyingi mke wake Shamsa Ford ndio amekuwa akiongea sana na waandishi au kuandika ktika kurasa zake za instagram kuhusu wao.
Chid Mapenzi , ikiwa hii ni moja ya mara chache alizowahi kufumguka, ameandika katika ukurasa wake wa instagram huku akiwa ameweka picha wa mke wake Shamsa Ford na kusema kuwa siku zote hekima ya mtu hainekani kwa kuongea sana au kunyamaza kimya lakini hata kama unaongea basi itapimwa kwa kile unachokiongea.
Hekima haipimwi kwa ukimya au uongeaji wa mtu bali kuongea mambo sahihi pale unapotaka kuongea na hata kukaa kimya pale unapopaswa kuongea.
Hivi karibuni wanandoa hao wamekumbwa na mkasa uliwaingia watu wengi lakini pia kumuingiza Chid Mapenzi baada ya kuweka katika list ya wanaume zaidi ya 10 waliowahi kutoka na Jackline Wolper kimapenzi , kitu ambacho yeye Chid mwenyewe hakutaka kukizungumzia tangu kimesemwa lakini mke wake alionekana kukwaza jambo hilo huku akisema kuwa baadhi ya mambo yalishapita hivyo hayakupaswa kuongelewa kwa wakati huu.
