Alikiba Apokea Tuzo ya Nyota wa Michezo.
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii Alikiba kutoa wimbo wake mpya wa mvumo wa radi, siku ya jana msanii huyo amepewa tuzo ya heshima kama nyota wa michezo kutoka katika kipindi cha The Playlist cha radio moja nchi ya Times fm.
Tuzo hitoaliokabithiwa Alikiba amepewa kama kuonyesha jinsi gani amekuwa akitambulika kwa mchango wake mkubwa wa kuipeperusha bendera ya taifa na pia jitihada zake alizokuwa akifanya mpaka sasa tangu alipoanza kwa kuwafanya wasanii wengine kutokata tamaa na kujituma ili kufanikiwa katika muziki huku yeye akiwa kama moja ya wasanii wanaoangaliwa kama mfano.
Times Fm walishawahi kutoa tuzo hiyo kwa wasanii wawili kabla ambao ni Vannesa Mdee pamoja na Diamond Platinmuz na sasa ni Alikiba.
