“Amber Lulu Ananiendea Kwa Waganga Kuniloga”- Amber Rutty

Msanii wa Bongo fleva aliyejizolea umaarufu kwa video yake chafu ya ngono kwenye Mitandao ya kijamii Amber Rutty ameibuka na kudai kuwa msanii mwenzake Amber Lulu anamuendea kwa waganga.

Amber Rutty na Amber Lulu wamekuwa hawana maelewano kwa muda mrefu ambapo kisa kilikuwa Amber Lulu aliona kama Amber Rutty anamuiga swaga zake kuanzia kumuiga jina na hata kumuiga tattoo zake alizochora mwilini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Amber Rutty amemtolea povu zito Amber Lulu na kudai amamuendea kwa waganga wa kienyeji kwa majaribio ya kutaka kumloga.

Amber Lulu amedai kuwa hawezi kumpenda Lulu kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa akijaribu kumshusha na kumharibia jina lake Lakini Baada ya kushindwa kwa njia hiyo sasa Hivi ameanza kumuendea kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kumloga asifanikiwe.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.