Aslay Akanwa Hadharani na Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva  Isihaka Nasorro maarufu kama Aslay anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nibebe’ amekanwa hadharani na Mrembo aliyeaminika kuwa na Mahusiano naye.

Mrembo huyo anayejulikana kama Diana Kimaro amekataa kata kata kuwa Kwenye Mahusiano na Aslay licha ya tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni wapenzi.

Tetesi za wawili hao kuwa Kwenye Mahusiano zilisambaa wiki iliyopita baada ya picha na video zilizowaonyesha wakiwa pamoja kusambaa Kwenye mtandao wa Instagram.

Kwenye mahojiano aliyofanya Kwenye kipindi cha U heard cha Clouds Fm, Diana amedai hamjui Aslay huku akienda mbali zaidi kwa kudai kwa sasa hayupo kwenye mahusiano.

Mimi sina mahusiano na mtu yeyeto, mbona huyo mtu simjui“.

Penzi la wawili hao lilizua gumzo hasa kwa sababu Aslay aliachana na Tessy aliyekuwa mpenzi wake siku chache zilizopita ambaye pia amezaa naye mtoto mmoja.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.