Babu Tale Atiwa Mbaroni.

Meneja wa kampuni ya Tip  Top Tanzania Babu Tale almaarufu amejikuta akiingia matatani baada ya kuwa anasakwa kwa muda mrefu huku sababu kubbwa ikiwa ni kesi inayohusiana na  kesi ya madai.Babu tale na mdogo wake Idd Taletale waliamuliwa kukamatwa na mahakama tangu tarehe  February 16 mwaka huu na naibu katibu msajili wa mahakama kuu baada ya kupokea kesi ya madai kutoka kwa  Sheikh Hashim Mbonde.

Hata hivyo tangu kulipotolewa mari hiyo ya mahakama Babu Tale na ndugu yake wamekuwa wakitafutwa na bila mafanikio ya kupatikana mpka walikamatwa siku ya May 21 mwaka huu na kupelekwa mahabusu moja kwa moja huku wakisubiri kuitwa tena mahakamani.

Mahamani kuu ambayo ilimuamuru babu tale kumlipa Sheikh Hashim Mbonde faini ya shilingi milion 250 za kitanzania kutokana na kesi ya madai baada ya kukutwa na hatia ya kutokuwa na hakimili ya kutumia masomo ya mhadhili huyo wa dini katika shughuli zao za kibiashara bila kuwa na ruhusa yake mwenyewe.

May 22 Babu Tale alifikishwa mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi hiyo iendelee na kusikiliza hukumu lakini kesi hiyo ilihairishwa na Babu Tale kurudishwa mahabusu kwa sababu  naibu msajili aliyetoa amri ya kukamatwa kwake kutokuwepo mahakamani hapo.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.