Baby Madaha Awatolea Uvivu Wanaume wa Kibongo

Msanii wa Bongo fleva Baby Madaha amewapa makavu ya Uso wanaume wa Dar na kudai ni Matapeli wa mapenzi.

Baby Madaha amefunguka na kuwatolea uvivu wanaume wa Kibongo huku akiweka wazi kuwa kutoka na wanaume hawa ni kujitia tu nuksi kwani huishia kukupotezea muda na kukutosa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers ,Baby  Madaha alisema kuwa watu wengi hawamuelewi kwa nini hawajawahi kumuona na mwanaume au kumnadi mpenzi wake mitandaoni kwa sababu hapendi kabisa kutoka kimapenzi na Mbongo.

Watakuja kunisikia tu nimeolewa huko nje ndio watajua ninachomaanisha, sipendi kabisa kumpa penzi Mmbongo kwa sababu wengi wababaishaji na wanajua kutiana nuksi sana kwakweli“.

Wanaume wa Kibongo nao wamekuwa wakisema hayo hayo mambo kuhusu wanawake hadi wengine hasa mastaa wa kiume wameonekana wakienda kuoa nje ya nchi kwa kuwakimbia watoto wa kike wa kibongo.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.