Baraka Awashauri Wasanii Wamuige Alikiba.
Msanii Baraka the Prince amefunguka na kuwataka wasanii ambao wanakipaji zaidi ya kimoja kuvitumia vipaji vya kwa ajili ya kujinufaisha na kupiga mkwanja kwa sababu kutegemea kipaji za muziki tu muda mwingine ni kufeli maisha.
Baraka anasema kuwa yeye ni mchezaji mzuri sana wa mpira wa kikapu na kama anaweza kupata nafasi ya kucheza basi atacheza timu yoyote itakayo mtaka huku akimtolea mfano msanii mwenzao alikiba ambae kwa sasa anafanya muziki na pia anaendeleza kipaji chake cha mpira wa miguu.
Baraka anasema kuwa kitendo cha baraka kujiingiza katika muziki kutoamuongeza amshabiki wengi wa muziki na wale wa mpira lakini pia hiyo inamuongezea kipato kwa sababu anakuwa anapata kote kote.
Hivi karibuni alikiba amekuwa akionekana akiwa na jezi ya timu ya Coastal Union na wamethibitisha kumsajiri msanii huyo kama mchezaji kwa kipindi hiki cha ligi.