BASATA Watoa Tamko Picha Chafu za Sanchi

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa tamko kuwa litamshug-hulikia mwanamitindo ambaye ni gumzo mtandaoni kwa kuposti picha za nusu utupu, Jane Rimoy ‘Sanchi’ baada ya malalamiko ya watu wengi ya kwa nini baraza hilo halimchukulii hatua kama ambavyo hufanya kwa wengine.

Akizun-gumza na Showbiz XtraAfisa Habari wa Basata, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita kumchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

“Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia,” alisema Agnes

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.