Beka Flavor Afunguka Mazito Kwa Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa Kwenye gemu Bakari Katuti maarufu kama Beka Flavor amefunguka mazito kwa mpenzi wake Sophia.

Beka Flavor alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la muziki lililofanya vizuri sana miaka ya nyuma Ya Moto Band na tangu ametoka Kwenye kundi hilo amekuwa akifanya vizuri sana.

Beka amefunguka na kusema anampenda sana mpenzi wake anayejulikana kama Sophia kiasi ya kwamba anatamani kumlinda kila wakati.

Kwenye Interview yake  na Ijumaa Wikienda , Beka Flavor alisema kuwa, amekuwa na mapenzi makubwa sana kwa mpenzi wake huyo kiasi ambacho anatamani kumuwekea ulinzi wa mbwa kila mitaa anayokatiza.

Mapenzi niliyonayo kwa Sophia wangu ni makubwa mno, natamani sana ningeweza kumlinda popote anapoenda awe na mbwa ili asisogelewe na mtu yeyote yule kwa sababu nampenda sana jamani”.

Lakini pamoja na maneno hayo matamu ambayo Beka ameongea kuhusu mpenzi wake Sophia lakini ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuoa kwa hivi sasa mpaka hapo baadae mambo yake Yatakapo kama vizuri.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.