Ben Pol Afungukia Mapenzi Yake Kwa Monalisa

Ben Msanii wa muziki wa RnB Bongo, Benard Paulomaarufu kama Ben Pol amefunguka na kuelezea jinsi anavuomkubali mwanamama Mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Ivyonne Cherry ‘Monalisa’.

Ben Pol ameweka wazi kuwa Monalisa ndiye mwanamke namba moja kwake kuliko wasanii wote wa kike wa muziki na filamu Bongo.

Monalisa ameonekana kama video queen katika video ya nyimbo mpya ya Ben Pol inayofanya vizuri hivi sasa ‘Ntala Nawe’.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ben Pol amefunguka na kuweka wazi kuwa anamkubali sana Monalisa kutokana na kazi zake Lakini pia amekuwa akimuhamisha kufanya Muziki bila kiki.

Ananihamasisha kwa kweli kwa namna anavyojitunza, nimefarijika sana kugundua kwamba Monalisa pia anapenda muziki wangu same way mimi ninavyopenda kazi zake za filamu, nilikuwa na ndoto ya kufanya kazi naye siku moja, nashukuru Mungu leo imetimia, niwaombe mashabiki waingie kwa wingi kujionea kazi yangu mpya katika Mtandao wa Youtube niliyofanya naye inayoitwa Ntala Nawe”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.