Carol Ndosi Aiandikia Jumuiya ya Afrika Kuhusu Hali ya Matukio Tanzania

Mwanadada Carol Ndosi na mjasiriamlai mbunifu wa Nyama Choma Festival amefunguka katika mitandao ya kijamii na kuweka wazi matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea Afrika hususani Tanzania  kwa kipindi hiki.

Akiwa kama moja ya wahamasisha wakubwa katika itandao ya kijamii kwa wanawake wengine na vijana kwa ujumla katika tasnia ya sanaa , siasa na hata maswala ya kijamii Carol anaamini kuwa warak huo unaweza kuleta madhara kwa jumuiya kimataifa.

Katika mtandao wake wa jamii forum , Carol Ndosi amefunguka na kuongelea kuhusu mauaji ya aAkwilina, utekwaji wa waandishi wa habari kama Azory  gGwanda na kesi ya Abdul Nondo na umwinywaji wa vyombo vya habari.

Carol amefunguka na kuwaambia jumuiya  hiyo kuwa hawawezi kujiita wadau wa maendeleo ya jamii ilhali wamekuwa wakiyafumbia macho mambo makubwa kama hayo.Carol anasema kuwa dhumuni la waraka ake sio kuomba msaada kwa jumuiya hiyo bali ni kuwapa tahadhari kuwa yasije yakatokea makubwa zaidi ya hayo nawakaanza kujuta kwamba kwanini hawakufanya zaidi kabla.

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.