Dayna Nyange Asafisha Nyota na Wizkid Nigeria

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye ni hitmaker wa Mafungu ya nyanya, Dayna Nyange amefunguka na kueleza jinsi alivyokutana na staa wa nchini Nigeria Wizkid.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Dayna amefunguka jinsi alivyokutana na Wizkid ambaye  alimpokea vizuri na hata sapoti kubwa aliipata kutoka kwa Wizkid.

Siwezi kusema kuwa nipo njiani kutoa naye wimbo, hiyo inabaki kimenejimenti kwa sasa lakini ninachotaka kushea na nyinyi, jamaa (Wizkid) ameweka heshima ya aina yake kwao, amekuwa ni mtu wa watu na hata nilivyokutana naye kila mmoja alikuwa akijiuliza huyu nani ametoka wapi, kumbe ni Mbongo mimi, haaa haaa.

Mbali na kukutana naye na kuzungumza naye mawili matatu, nilibahatika kutembelea redio zao, yaani karibu kila redio ni kama wameweka kautamaduni kao, kuna picha kubwa za wasanii wao wanaoiwakilisha nchi, kuna P Square, Wizkid, Davido, Yemi na wengine wengi tofauti na hapa Bongo kikubwa utakutana na saini za wanamuziki tu”.

Dayna ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ameachia ngoma yake mpya ya ‘Salama’ ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.