Diamond: Ilibidi nipunguze kasi nyimbo zangu zisiwaue kina Harmonize, Rayvanny

Diamond ameeza kwanini alikosa kupata uteuzi wa tuzo la BET mwaka huu. Hit maker huyo wa ‘Marry You’ amewahi kuteuliwa mara mbili (2014 na 2016) kuwania tuzo hilo kwa kitengo cha Best International Act: Africa.

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alieleza kuwa alipunguza kasi yake kimuziki mwisho wa mwaka jana ili akuze kina Rayvanny, Harmonize na wasanii wengine.

Alieza kuwa msanii kupata uteuzi wa BET ni lazima aachilie nyimbo mfululizo na yeye aliwacha kutoa ngoma nyingi kwani kama angefanya hivyo nyimbo zake zingewaua kina Harmonize, Rayvanny na wengine.

“Mwakani lazima niingie, unajua kuna kitu kimoja…lazima uishi kwa plani na malengo…Na ukiangalia mwaka juzi mwishowe mbaka mwaka jana ulikua ni mwaka kuhakikisha nawashika vijana wa Kitanzania nao wasikike katika muziki. Na ili wasikike ilibidi mimi nipunguze kasi yangu kwasababu mimi naachilianga tu mawe, ilibidi nipunguze mawe niwashindirie tu hao mawe kina Harmonize, sijui kina nani Ray… wote…kwasababu nikiingia itakua ni mtafaruko. Ukiangalia mitaa ingine nimeanzisha lebo kuna nyimbo kama tatu, nyimbo zangu zingine ni mishirikisho tu. Ilibidi nipunguze kwasababu mimi najua nikiweka nyimbo na hawajakua na nguvu nyimbo zangu zitawaua. Na zile nomination zinataka mtu aachilie ngoma mfululu,” Diamond alisema.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=K_fRN6xFS8o

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.