Diana Edward Avutiwa na Ali Kiba

Mrembo aliyewahi kushindwa Miss Tanzania mwaka 2016, Diana Edward amefunguka na kuelezea hisia zake kwa msanii wa bongo fleva Ali Kiba kuwa ndie anaevutiwa nae muda wote na sio wasanii wengine wa kiume ambao hawatulii kama Ali Kiba,

Diana amesema kuwa msanii huyo yuko tofauti na wasanii wengi wa kiume bongo kwa sababu muda wote amekuwa akifanya mambo yake yanayomhusu hata kubishana na watu katika mitandao inakuwa ni nadra sana hivyo anamuona ni msanii wa kiume wa tofauti.

Akiongea na planet bongo ya East Afrika Radio, Diana Edward anasema kwake yeye ali kiba ndio msanii pekee anaemuona ametulia kwa sababu yuko kivyake vyake.

Tatizo watanzania ni mabingwa wa kubadili vitu sana, ukiongea hivi na wao wanasema hivi lakini kiukweli msanii wa kiume ninaempenda tanzania ni Alikiba,nampenda kwa sababu nadhani ametulia sana kuliko wasanii wote wa kiume bongo.najua wengi wametulia lakini mimi ninamuongelea yeye kwa sababu huwa haweki mambo yake wazi sana kama wengine hivyo ndo maaa mimi ninampenda sana Ali Kiba.

                                                

                                                           ali kiba

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.