Diva Alia Kukosa Mtoto, Awaomba Watanzania Wamchangie Milioni15

Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva The Bawse amefunguka na kueleza kuwa anahitaji mchango wa kiasi cha dola $7,000 ambazo ni sawa na milioni 15 za Kitanzania, kwa ajili ya matibabu ya kumsaidia kushika mimba.

Diva amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa mwezi uliopita alienda Hospitali ya TMJ kufanya vipimo na aliambiwa kuwa mirija yake ya uzazi ina hitilafu (blockage) hivyo hawezi kutunga mimba kwa njia ya kawaida mpaka kwa mfumo wa kisasa wa kupandikiza mbegu wa IVF Treatment.

Diva amesema kuwa anajua kuna wanawake wengi wenye matatizo kama yake hivyo kufanya hivyo kutawafanya na hao wapate nafuu na kutambua kuwa tatizo hilo ni kubwa kwenye jamii Lakini pia ameomba kuchangiwa kupitia akaunti yake ya Go Fund me na akaunti ya benki.

https://www.instagram.com/p/Bmro7lBlMzA/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=eeg3cvxfu0ss

 

https://www.instagram.com/p/BmrqMyVluqP/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1hqz5l0xipo0r

 

https://www.instagram.com/p/Bmrq7EylF5p/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17w1bkawga15d

 

https://www.instagram.com/p/BmsCnu2F1vl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=12klthh8hclxk

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.