Diva Amefunguka Haya Kuhusu Mpenzi Wake

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds FM Loveness Malinzi au maarufua kama Diva The Bawse amefunguka kuhusu mahusiano yake mapya.

Ikiwa ni miezi michache imepita tangu Diva na aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki waachane  hatimaye Diva ameweka wazi kuwa yupo na mpenzi wake mpya.

Wiki chache zilizopita Diva alishangaza watu wengi baada ya kutangaza kuwa hatakubali kuolewa kwa mahari isiyopungua milioni  500 kiasi cha fedha ambacho kimeonekana kingi kwa wengi.

Lakini pia Diva alitangaza kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa mwaka huu hata iweje lazima atahakikisha anazaa mtoto ingawa swali la watu wengi lilikuwa kama kaachana na mpenzi wake anazaa na nani?.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amewajulisha mashabiki zake kuwa tangu ameachana na Heri Muziki amepata mpenzi mpya na hiki ndicho alichoandika kuhusu mpenzi wake:

Mpenzi wangu mpya sio mtu maarufu wala sio mtu wa media wala movies..He is living in a cooperate world na kama nilivyosema sitaki mapenzi ya mtandao wala public Tena”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.