Dkt.Tulia Akson Ashindwa Kuficha Hisia Zake Kwa Kivuruge

Naibu spika wa  bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Akson ameshindwa kuficha hisia zake kwa  kuonyesha kuwa wimbo mpya wa Nandy wa kivuruge umekuwa gumzo mtaani na yeye ameupenda na kuupokea vizuri wimbo huo.

Dkt.Tulia amemsifia Nandy na kumwambia kuwa jitihada alizonazo katika muziki atafika mbali ukizingatia yeye ni msanii mchanga lakini ameweza kufanya muziki vizuri na watu wakamkubali.dkt tulia bado amemsifia nandy na kumwambia kuwa amefanya vizuri katika wimbo wa kivuruge kwa kitendo cha kuelezea malalamiko ya mwanamke anaeteswa na  mwanaume.

Kwa jitihahada hizi ninatumaini utrafika mbali sana, uvumilivu na nidhamu ni vitu vya kuzingatia sana kwenda  kwenye mafanikio yako.Wimbo wa kivuruge tumeupokea kwa mikono miwili. –  Aliandika dkt tulia katika ukurasa wake wa instagram.

Wimbo wa kivuruge ulitoka kama zawadi kwa mashabiki wa Nandy baada ya kushindwa tuzo huko nchini Nigeria, ambapo ulianza na audio na baadae kufuatwa na video.Ikiwa leo ni siku ya tisa tangu kutoka kwa video hiyo ilishatizamwa zaidi ya mara  600,000.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.