Dogo Janja Amlipizia Irene Uwoya
Kama mwezi tangu umepita Irene Uwoya alipoamuakuchora tatoo ya mume wake dogo janja kwa kuandika jina la Abdul ambalo ndio jina halisi la msanii huyo, mwanamuziki huyo nae ameamua kumjibu mke wake kwa kuchora tatoo sehemu yake ya mkono na kuandika jina zima la mke wake.
Dogo Janja na Irene Uwoya wamekuwa waki-trend sana katika mitandao kutokana na mambo yao ya kimapezni wanayoyafanya huku wakiwakosha mashabiki wao wengi na kuwapenda watu hao.
Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa mwaka uliopita huku ndoa yake ikiwa na maneno mengi kutokana na umri mkubwa wa mwanamke ambae Dogo Janja aliamua kumuoa na kwamba wengi walisema kuwa ndoa hiyo haitaweza kudumu kutokana na drama na aina ya watu ambao walikuwa wakiwafikiria lakini kitu cha ajabu ni kwamba wawili hawa wamekuwa wakionyesha kupendana pamoja na maneno mengi ya mitandaoni.