Faiza Ally Amjia Juu Mke Wa Sugu Baada Ya Kupiga Picha na Mtoto Wake

Msanii wa filamu za kibongo Faiza Ally ambaye pia ni mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, amemjia juu Mke wa Sugu baada ya kupiga picha na mtoto wake.

Faiza amerudi Kwenye headlines baada ya povu lake  siku ya jana kupitia mtandao wa Instagram ambapo Mke wa Sugu aitwaye Happy, alipiga picha ndani ya ndege na mtoto wa Sugu na Faiza Sasha wakati akimtudisha Jijini Dar.

Basi baada ya Faiza kuona picha hizo aliyekuwa mbogo na kumvaa Mke wa Sugu ambapo alimtuhumu kwa kupiga picha na mtoto wake ili apate kiki na kudai hana mapenzi ya kweli kwa mwanaye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliandika maneno haya:

Faiza na Sugu wamekuwa Kwenye vita za mitandao ya kijamii mara kwa mara huku Faiza akimtuhumu mzazi mwenzake kwa kugoma kutoa pesa za matunzo huku akimlaumu Mke wa Sugu kama chanzo cha yote.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.