Feza Kessy: Napenda Kulazimisha Mapenzi

Mwanamuziki wa Bongo fleva ambaye pia ni mtangazaji wa stesheni ya redio ya Choice Fm amefunguka na kukiri kuwa kwenye maisha yake huwa ana tabia ya kulazimisha mapenzi yotokee kwa mwanaume ambaye hakumpenda.

Feza amefunguka hayo baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la ‘Kaa kijanja’ ambao amemshirikisha rapa Nikki wa pili. Feza amekiri maana na stori ya wimbo huo inasadifu maisha yake kwani aliwahi kumpenda mwanaume ambaye kwa bahati mbaya hakuwa na muda naye.

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni Feza alifunguka na kusema:

Napenda kulazimisha vitu vitokee lakini  kwenye mapenzi hapana kwa sababu kuna mtu nilikuwa namlazimisha kimapenzi lakini kiukweli hakuwa upande wangu kitu kilicho nikatisha tamaa kwani mtu huyo niliyempenda yeye alikuwa akinisaliti kimapenzi”.

Feza alijipatia umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka 2013  baada ya kushiriki shindano la Big brother Africa ambapo alikuwa mmoja kati ya washiriki kutoka Tanzania.

Wiki chache zilizopita Feza alikiri kumtongoza Cyril Kamikaze na kwa muda walisemekana kuwa na mahusiano lakini wawili hao waliishia kumwagana.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.