Flaviana Matata Foundation Yatoa Vifaa Mashuleni.

Mwanadada ambae amefanikiwa sana katika kazi zake za mitindo Flaviana matata kupitia foundation yake wameweza kufanikiwa kutoa misaada kwa watoto wa shule ya msingi mzinune kwa kuwapa vifaa vya shule kwa mwaka 2019.

katika ukurasa wake wa instagram, Flaviana amenadika kuwa amefanikiwa kuwapa wanafunzi 284 wa shule hiyo ili waweze kwenda shuleni kwa mwaka mpya wa masomo.

Flaviana ameandika >>>”Leo muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019 umeanza. Taasisi yetu @flavianamatatafoundation ambayo ni walezi wa Shule ya Msingi Msinune tunaendelea na utaratibu wetu wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima”

“Kwa mwaka 2019, watoto 284 wa Shule ya Msingi Msinune kila mmoja kapata begi la shule, kalamu za wino 50 , kalamu za risasi 50 na vifutio ambavyo vitakidhi mahitaji yao kielimu kwa mwaka huku wazazi wakitimiza mahitaji mengine yaliyobaki. Upande wa walimu taasisi imetoa kalamu, chaki, rejista za masomo na karatasi (reams) kwa ajili ya kudurufu (copy) mitihani na kazi za masomo”

 

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.