Hamisa Mobetto Amfungulia Kesi Ya Madai Diamond

Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia Kesi ya madai mzazi mwenzie Diamond Platnumz kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao Abdul Naseeb Juma.

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Hamisa Mobetto Abdullah Zullu na Walter Goodluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili huyo alipozungumza na gazeti la mwananchi amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika mahakama ya kisutu upande wa mtoto (The Juvenile Court of Dar es Salaam) na Leo tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea”.

Diamond alikiri kuzaa na Hamisa mwezi uliopita na kudai anatoa pesa kubwa kwa ajili ya malezi ya mtoto wake kitu ambacho Hamisa amepinga na kudai hajatoa pesa yoyote tangu mtoto amezaliwa miezi miwili iliyopita.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.