Harmonize aeleza hofu aliokuwa nayo na uamuzi wa lebo ya WCB Wasafi

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Harmonize alisema alikuwa na hofu na  lebo ya WCB Wasafi baada ya uongozi wake kumtaka kuachia wimbo wake mpya kwenye tovuti ya Wasafi.com badala ya kuachia kwenye TV na redio kama ilivyo desturi.

Harmonize alikiri kuwa alidhani WCB Wasafi walitaka kumpoteza katika ramani ya muziki ndiyo maana hawakutaka atangulize wimbo wake mpya kwenye TV na redio.

Ata hivyo Harmonize amefurahia uamuzi huo, anasema kuwa wimbo wake umepokelewa vizuri na mashabiki wake kwenye tovuti ya Wasafi.com.

“Unajua mimi WCB ni kama chambo kwa sababu hata lebo ilipoanzishwa mimi ndiye niliyekuwa msanii wa kwanza kusaini na nikafanya vizuri wengine wakaja, hata hivyo kwenye mauzo ya muziki kwenye mtandao nimetangulizwa mimi na namshukuru Mungu kazi zimepokelewa vizuri. Uongozi ulikuwa na mtazamo chanya tofauti na nilivyowaza,”alisema Harmonize.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.