Harmonize Ajivunia Kwangaruu Nchini Kenya.

Msanii wa muziki kutoka katika kundi la WCB anajivunia kufanya vizuri kwa wimbo wake wa kwangaru ambao alimshirikisha bosi wake Diamond Platinumz.

Harmonize ambae yuko nchini humo kwa ajili ya kufanya tour ya wimbo huo anasema  katika kila sehemu anayofanya show anaona kuwa na mwitikio mkubwa na mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.

Harmonize anafurahi zaidi anapoona kuwa kila anapopanda jukwaani kuimba wimbo huo , mashabiki wamekuwa wakiuimba mwanzo mwisho, kitu kinachompa matumaini zaidi.Na hata baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa wimbo huo ndio wimbo wa mwaka.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.