Harmonize Amvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake Sarah

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Kwangwaru’ Harmonize amemvalisha Pete ya uchumba mpenzi wake mwenye asili ya Italia Sarah Michelotti.

Harmonize na Sarah walikuwa kwenye mgogoro wiki chache zilizopita baada Sarah kumtuhumu mpenzi wake huyo kwa kuchepuka baada ya kuona picha zake na mtangazaji kutoka Nigeria Nancy Isime na kudai ni wapenzi.

Lakini Sarah na Harmonize walionekana kumaliza tofauti zao siku chache zilizopita baada ya kuonekana pamoja Kwenye shoo  ya Kusi Night wakiwa wanakumbatiana stejini.

Hatimaye wawili hao wameweka wazi kuwa wamechumbiana baada ya Kuposti video iliyomuonyesha Harmonize akimvalisha Sarah Pete na Sarah Kuposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram na Kuandika “Thank You Baby ♥️“.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.