Harmonize Awasaidia Walemavu Dar

Msanii kutoka katikakundi la WCB,Harmonize ameamua kuchukua uamuzi wa kuwasaidia watu wenye uhitaji hasa walemavu wanaoshindwa kutembea kwa kuwapa viti kwa ajili ya kutembelea.

Harmonize amefanya hivyo kwa watu hao akiamini kuwa hata watu hao pia ni mashabiki zake na wanahitaji kupata shukrani zake kwa fadhila ya kumsapotu kila siku katika maisha yake ya muziki.

Katika ujumbe alioandika mzito na mrefu Harmonize anasema kuwa amekuwa koja ya watu wanaosapotiwa sana na ni jukumu lake basi kufanya hivyo kwa watu wanaomjali pia.

Harmonize anakiri kuwa mwaka 2018 umekuwa mwaka wake wenye mafanikio sana hivyo haoni jasara kuamua kutoa shukrani na misaada kwa watu waliomfanya kufanikiwa katika mambo yake hasa muziki ambao kwake ni kazi.

Hii sio mara ya kwanza kwa msani Harmonize na hata kutoka WCB kuwa wakitoa misaada kwa wahitaji katika jamii.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.