Harmonize awataja warembo wawili kutoka Kenya ambao wanampendeza sana

Harmonize alisafiri kuenda Nairobi, Kenya kupigia upato nyimbo zake. Staa huyo kutoka Wasafi Records WCB amefanya mahojiana na vitua vya habari kadhaa jijini Nairobi.

Katika mahojiano na kipindi cha Mambo Mseto ya Radio Citizen hapo jana, Harmonize aliulizwa kumtaja mrembo kutoka Kenya anayemgusa sana.

Mzazi Willy Tuva na Harmonize wakiwa Citizen Radio

Harmonize alicheka na kuwaza kwa sekunde chache kabla ya kusema kwamba Kenya iko na watoto wazuri wengi.  Hata hivyo alisema Huddah Monroe and Vera Sidika ndo wanampendeza sana.

“Suppose kama haugekuwa na Wolper alafu ibidi uwe na mchumba hapa Kenya ni mrembo mgani wa humu nchini Kenya ambaye huwa ana ‘Kugusa’ kinyama?” Harmonize aliulizwa.

“Kenya kuna watoto wazuri kabisa… …mtoto VERA hivi…. mtoto MONROE hivi….wako wengi bana, wote wako sawa,” alijibu Harmonize.

Huddah Monroe

 

Vera Sidika

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.